0:00
4:32
4:32

JEMEDARI SAID KAZUMARI AMVAA CLATOUS CHAMA, MAHOJIANO YAKE NA FATMA DEWJI YANA MAKOSA HAYA KISHERIA

Sports

#jemedarisaid #clatouschama #Yangasc SIMBA SC KWA MARA NYINGINE IMEONYESHA UDHAIFU WA KIUTENDAJI. Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 inakataza mtu ambaye sio mwana taaluma ya habari kufanya kazi za kitaaluma. Sheria hii iliundwa ikiibadili iliyokuwa inaitwa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976. Kufanya mahojiano (interview) kwa namna alivyokuwa anafanya Fateema Dewji ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kwakuwa yeye si mwana taaluma na hana ithibati. Nataka kuamini CEO wa Simba SC Bi Zubeda Sakuru kwa usomi wake na kuwahi kwake kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anajua hili ni jambo la hovyo kiasi gani. Kuruhusu mfanyakazi/mwajiriwa wake kuwa sehemu ya kuvunja Sheria ni kosa kiasi gani, lakini hata kuruhusu mtu ambaye sio mwana taaluma kufanya mahojiano na mchezaji ni kitu cha hovyo kiasi gani. Klabu kubwa kama Simba ambayo ni klabu namba 1 kwa Ubora Tanzania kwa mujibu wa CAF (Simba namba 11 & Yanga namba 12), kujiingiza kwenye uvunjifu wa sheria na taratibu za nchi ni kitu cha hovyo na kinachafua taswira nzima ya klabu hii kongwe nchini. Ifike hatua watu wawe smart na kufanya majukumu yao, kuweka uchawa kando na kusimamia Taasisi kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na misingi iliyounda na kusimamia Taasisi wanayoinogoza, Simba SC ni Taasisi kubwa na yenye heshima Afrika, hapa wamejishusha sana. BIN KAZUMARI MTIPA (Voice of the Voiceless)

ADVERTISEMENT
Comments 0 Be the first to comment